The piece below is by Mombasa based Music producer and stakeholder Khalid.
Unapozungumzia sanaa,unazungumzia kiwanda cha uzalishaji,sawa na viwanda vyengine. Tofauti ni kuwa kiwanda hiki ni uzalishaji wa ubunifu kutoka kwa watu tofauti tofauti. Kiwanda hiki kukuwa, ni sharti washikadau wote wawe na ari moja,nia na nguvu zote zielekezwe kuinua,kujenga,kuwekeza na kuitunza sanaa kwa vizazi vijavyo.
Sanaa imeajiri vijana wengi,hivyo basi kukimu mahitaji yao na pia ya familia. Unapozungumzia sanaa basi moja kwa moja unazungumzia maisha ya maelfu ya watu,unazungumzia ajira,kitega uchumi na pato kwa serikali kama ushuru.
Hivyo basi matamshi ya Makku presenter wa pwani fm kusema Mombasa hakuna msanii mzuri na wasanii wote wanaimba vitu havieleweki,ni kuikejeli na kuibeza sanaa ya Mombasa na Matamshi yake niyakupotosha. Naamini ameongea hivyo kwasababu hajui sanaa ni nini,hajui chochote kuhusu mziki wa pwani,naamini pia wasanii wa pwani hawajui. Pia naamini hajahitimu vizuri kuwa mtangazaji. Hawa niwale wakuokotwa na kuwekwa.
Kama Dully sykes ni shabiki wa mziki wa Mombasa. Itakuwaje yeye hajui lolote. Najiukiza maswali mengi sana. Je maneno yake ndio msimamo rasmi wa Pwani fm? Kwasababu anachokiongea akiwa on air basi moja kwa moja anawakilisha stesheni. Na kama sio msimamo wa stesheni,je wamechukua hatua gani kwa sababu matamshi yake yameudhi wengi. Hivi kuna wasanii wa pwani bado anawafanyia interview? Sasa utaalika vipi msanii mwenye anaimba vitu havieleweki na hana mziki mzuri. kivipi umueke on air na kucheza nyimbo zake ?
Na kama wataalika wasanii wa pwani, kwa interview na kucheza nyimbo zao. Basi hiyo stesheni pia haijui inachokifanya na wao pia wamechanyikiwa.
Kuna wasanii wengi tajika pwani,waliokuwepo na waliopo ambao bado wanapeperusha bendera ya pwani kwenye anga za africa mashariki. Kuanzia kwenye bendi za Safari sound,Pressmen band,Them mushrooms,Mzee ngala mwenyewe. Wasanii kama kina Malikia rukia,Poxi presha, Kingsting & bedbug,prince adio,Nyota ndogo,Ali B,Susumila,Masauti,Kelechi, Sudi boy,Jovial,etc Kwa miaka zaidi ya 30, sanaa ya mombasa imekuwa iking'aa japo kwa mwangaza wa tochi. Kivyovyote vile huwezi kukejeli mziki wa hawa wasanii.
Hivyo basi kwa kukejeli hawa wasanii wakiwa tu ni baadhi yao,anafaa kuchukuliwa hatua. Afutwe kazi au aombe msamaha. Kama tutatumia kigezo cha 'freedom of speech', basi ameiharibia jina pwani fm walilolijenga miaka mingi. Na yeye mwenyewe amejijengea chuki kwa mashabiki wa mziki wa pwani,wasanii,mameneja wa wasanii,waandaji wa matamasha,promoters, DJs na presenters wenye wanatumia nguvu nyingi kuuskuma mziki wa mombasa.